Uturuki yakubali mapatano na Israel

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uhusiano baina ya Uturuki na Israel ulivunjika miaka sita iliyopita

Bunge la Uturuki, limekubali mapatano yaliyotiwa saini na Israel mwezi Juni.

Uhusiano baina ya Uturuki na Israel ulivunjika miaka sita iliyopita, pale makamando wa Israel, walipowauwa wanaharakati 10, waliokuwa ndani ya meli ya Uturuki, iliyokuwa ikielekea Gaza ikiwa na shehena ya msaada.

Kufuatana na makubaliano hayo, Israel italipa fidia ya dola milioni 20, na miradi ya Uturuki ya kupunguza shida za Gaza, itaanza.

Mbunge mmoja wa Uturuki wa chama tawala cha AKP, Burhan Kuzu, alisema makubaliano hayo yatanufaisha Israel kwa sababu kadha.