Uturuki yaidhinisha mapatano na Israel

Rais Reccep Tayyip Erdogan
Image caption Rais Reccep Tayyip Erdogan

Bunge la Uturuki limeidhinisha mapatano ya amani kati yake na Israel kama yalivyotiwa saini mnamo mwezi Juni, mwaka huu.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulivunjika miaka sita iliyopita wakati makomando wa Israel walipowaua wakereketwa 10 kutoka Uturuki waliokuwa kwenye meli ya kupeleka misaada eneo la Gaza.

Chini ya mkataba wa amani wa sasa Israil italipa fidia ya Dola Milioni 20 na miradi ya kibinadamu iliyoanzishwa eneo la Gaza itaruhusiwa kuendelea.

Image caption Benjamin Netanyahu

Tayari baraza la mawaziri la Israel limeidhinisha mpango huo.

Awali Uturuki ilitaka kumalizika kwa kizuizi cha kuingiza bidhaa eneo la Gaza kiondolewe lakini kwa sasa kitasalia kilivyo.

Mada zinazohusiana