Korea Kaskazini yawataka raia wake kurudi nyumbani

Wafanyikazi wa Korea Kaskazini waliohamia Korea Kusini
Image caption Wafanyikazi wa Korea Kaskazini waliohamia Korea Kusini

Korea Kaskazini imelitaka kundi la wafanyikazi wa mkahawa mmoja waliohamia nchini Korea Kusini mapema mwezi huu kurudi nyumbani.

Wito huo ni hatua ya kwanza ya taifa hilo kufuatia tangazo la maafisa wa Korea Kusini kwamba kundi hilo limeachiliwa huru.

Wafanyikazi hao waliamua kuhamia nchini Korea Kusini mnamo mwezi Aprili kutoka mkahawa mmoja wa Korea Kaskazini katika mji wa kichina wa Ningbo.

Korea Kaskazini inasisitiza kuwa kundi hilo lilitekwa nyara na huduma ya kitaifa ya ujasusi ya Korea Kusini,lakini Korea Kusini inakana hilo ikisema raia hao walihama kwa kupenda kwao.

Mada zinazohusiana