Upinzani DRC wakataa mazungumzo ya AU

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani DRC
Image caption Wafuasi wa kiongozi wa upinzani DRC

Muungano mpya wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umekataa jaribio la mwisho la Umoja wa bara Afrika kuanzisha mazungumzo ya kitaifa.

Katika taarifa yake iliotolewa baada ya mkutano wa dharura ,kundi hilo limemshtumu mpatanishi wa Umoja wa Afrika Edem Kodjo ambaye linadai anataka kuhakikisha kuwa rais wa sasa Joseph Kabila anawania muhula wa tatu,swala linalokiuka katiba ya taifa hilo.

Kundi hilo sasa limeitisha mgomo siku ya Jumanne,siku ambayo bwana Kodjo,waziri mkuu wa zamani nchini Togo alitaka mazungumzo hayo kufanyika baada ya serikali kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa.

Image caption Rais Joseph Kabila

Uchaguzi ulitarajiwa kufanyika mwezi Novemba ,lakini umecheleweshwa na mahakama kuu ya DRC ambayo imesema kuwa rais Kablia ataendelea kuongoza hadi pale uchaguzi utakapofanyika.

Mada zinazohusiana