Shambulio la al-Shabab lawaua watu 10 Somalia

Wapiganaji wa al-Shabab
Image caption Wapiganaji wa al-Shabab

Zaidi ya watu 10 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika makao makuu ya serikali ya taifa lilolojitenga kutoka Somalia la Puntland.

Walioshuhudia wanasema kuwa mabomu mawili yaliotegwa ndani ya magari yalilipuliwa yakifuatana nje ya ofisi katika mji wa Galkayo.

Milio ya risasi ilisikika.

Maafisa wa usalama pamoja na raia ni miongoni mwa waathiriwa.

Kundi la al-Shabab limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Kundi hilo limefurushwa katika maeneo mengi ya miji nchini Somalia,lakini linaendelea kufanya kampeni dhidi ya serikali na kuwalenga raia,mbali na vikosi vya Umoja wa Afrika vinavyounga mkono serikali.

Mada zinazohusiana