Mfalme wa Morocco awataka Waislamu kupuuzilia mbali itikadi za kidini

Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita
Image caption Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita

Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita, amewaomba raia wa nchi hiyo wanaoishi ughaibuni, wengi wao walioko barani Ulaya, kutetea dini ya Kiislamu na kupuuzilia mbali itikadi kali za kidini.

Ni mara ya kwanza kwa Mfalme Mohammed, kuwahutubia raia milioni tano wa Morocco wanaoishi nje ya nchi, kufuatia visa vya hivi majuzi vya mashambulio ya kigaidi barani Ulaya na Waislamu wenye itikadi kali.

Baadhi ya raia wa bara Ulaya wenye asili ya Morocco, wametuhumiwa kuhusika na baadhi ya mashambulio hayo.

Mada zinazohusiana