Wapiganaji 36 wa Islamic State wanyongwa Iraq

Makuruti waliouawa na wapiganaji wa Islamic State 2014
Image caption Makuruti waliouawa na wapiganaji wa Islamic State 2014

Iraq imewanyonga wapiganaji 36 wa kundi la Islamic State wanaohusishwa na mauaji ya makurutu 1,700 katika kambi moja iliokuwa ya Marekani mwaka 2014.

Mauaji hayo katika kambi ya Speicher karibu na Tikrit yalifanywa na wapiganaji kutoka Islamic State ilipochukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa Iraq.

Hisia kali zilizotolewa kufuatia mauaji hayo ya raia wa Kishia zilichochea kubuniwa kwa kundi la wapiganaji wa Kishia katika vita dhidi ya Islamic State.

Wapiganaji wa Islamic State walitoa picha na video wakionyesha mauaji hayo ya 2014.

Makaburi ya halaiki yalifichuliwa mwaka mmoja baadaye.

Makaburi hayo yaligunduliwa baada ya wanajeshi wa Iraq kulikomboa eneo hilo.

Mada zinazohusiana