Rais wa Ufilipino atishia kuondoka UN

Rais wa Ufilipino Rodrigo Durtete
Image caption Rais wa Ufilipino Rodrigo Durtete

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, ametishia kuliondoa taifa lake kutoka Umoja wa Mataifa, baada ya Umoja huo kumshutumu kuwa anakiuka sheria za kimataifa, kwa kuendeleza kampeini yake dhidi ya magenge yanayohusika na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Kampeini hiyo mpya imeshuhudia mauwaji ya watu wengi wanaotuhumiwa kuhusika katika biashara hiyo haramu.

Rais Duterte amesema kuwa ni hekima ipi iliyotumika na umoja wa mataifa kusikiza mapendekezo ya shirika moja analoliita la " kijinga".

Amesema kuwa anapania kuiondoa Ufilipino ndani ya uanachama wa Umoja wa Mataifa na badala yake kuialika Uchina na mataifa ya Afrika kujiunga pamoja na kubuni muungano mwingine mbadala wa kimataifa.

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 800 wameuawa na polisi na makundi ya vijana ya kupambana na mihadarati tangu Rais Duterte aliposhinda uchaguzi mkuu mwezi Mei mwaka huu.

Mada zinazohusiana