Mwanamuziki azuiliwa kwa 'kutusi Uislamu' Malaysia

Mwanamuziki wa Malaysia Namewee Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamuziki wa Malaysia Namewee

Polisi wamemkamata mwanamuziki maarufu wa kutatanisha wa Malaysia baada ya malalamiko kutoka kwa raia kuhusiana na wimbo wake wa hivi karibuni unaokisiwa 'kuwatusi waislamu'

Namewee, 33, ambaye jina lake rasmi ni Wee Meng Chee alikamatwa siku ya Jumapili katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur huko Malaysia.

Video hiyo kwa jina Oh My God, ambayo inadaiwa kuudhi, ilizinduliwa rasmi mwezi Julai ambapo mwanamuziki huyo anaonekana akiimba kwa kutumia mtindo wa kufoka mbele ya msikiti nchini Malaysia.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mzozano wa kidini nchini Malaysia

Mwanamuziki huyo wa mtindo wa Rap, Namewee alisisitiza kwamba wimbo huo wa Oh My God una madhumuni ya kukuza maelewano ya kidini.

Polisi wamesema wamemkamata na atazuiliwa kwa siku nne kuchunguza iwapo mwanamuziki huyo 'aliichafua' sehemu hiyo ya maombi kimakusudi ili kuitusi dini hiyo.

Akipatikana na hatia, huenda akafungwa jela hadi miaka miwili

Takriban robo tatu ya raia wa Malaysia ni Waislamu, ingawaje kuna dini kama vile za Kikristo, Kihindu na Kibudha