Mwanahabari wa Burundi Eloge Willy Kaneza ashinda tuzo ya kimataifa

Machafuko nchini Burundi yaliyoshuhudiwa mwezi Mei mwaka 2015 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Machafuko nchini Burundi yalizidi mwezi Mei mwaka 2015 baada ya kutokea jaribio la mapinduzi ya serikali

Mwanahabari wa Burundi ameshinda tuzo la kimataifa la kwa kuwa mwanahabari mkakamavu na jasiri.

Eloge Willy Kaneza na wanahabari wenzake walipata njia bora za kukabiliana na ukandamizaji kwa kutumia mfumo ya teknolojia za kimitandao, waandalizi wa tuzo za Peter Mackler za wanahabari wakakamavu na wenye maadili walisema.

Bw Kaneza Eloge,34, ni kioo cha muungano wa wanahabari wa SOS nchini Burundi, uliobuniwa baada ya vituo vingi vya habari kufungwa mwezi Mei mwaka 2015 baada ya kutekelezwa kwa jaribio la mapinduzi ya serikali ya Rais Pierre Nkurunziza.

Wanahabari hao walitumia simu za rununu aina ya Smartphone, na kufanya kazi katika hali ngumu ili kuwa chombo cha habari kwa raia waliokuwa ndani na nje ya Burundi, waandalizi walisema.