ANC chabwagwa uchaguzi wa Meya Johannesburg Afrika Kusini

Democratic Alliance kwa sasa kinashikilia baadhi ya miji mikubwa nchini humo
Image caption Democratic Alliance kwa sasa kinashikilia baadhi ya miji mikubwa nchini humo

Chama tawala nchini Afrika kusini ANC kimepoteza udhibiti katika jiji la Johannesburg ambapo meya mpya wa jiji hilo Herman Mashamba anatoka chama cha upinzani cha Democratic Alliance.

Chama cha ANC kipo madarakani tangu kipindi cha ubaguzi wa rangi nchini humo zaidi ya miaka 20.

Mashamba ameahidi kubadilisha utawala wa jiji.

ANC ilipoteza majimbo mengi katika uchaguzi wa mwezi uliopita lakini bado ni chama kikubwa na kikongwe nchini humo.