Wapenzi wa jinsia moja 'wajifungua' watoto 3 Afrika Kusini

Wapenzi wa Jinsia moja wakiwa na mtoto wao
Image caption Wapenzi wa Jinsia moja wakiwa na mtoto wao

Wapenzi 2 wa jinsia moja nchini Afrika Kusini wanaaminika kuwa wa kwanza duniani kujifungua watoto watatu kutoka kwa vinasaba vya DNA vya wanaume hao wawili ,kulingana na jarida la Gay Times.

Mnamo mwezi Julai mama aliyebeba mimba ya watoto hao ambapo wawili ni mapacha alijifungua -kakitendo kisicho kuwa cha akawaida.

Jarida hilo linasema kuwa kwamba wapenzi hao wa jinsia moja walikutana na mama aliyebeba mimba hiyo kupitia mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ambaye ni jirani wao.

Christo na Theo Menelaou alikutana na mama aliyebeba mimba hiyo katika sherehe ya kuwaleta pamoja marafiki na ndugu za Oscar Pistorius baada ya kesi ya mwanariadha huyo .

Mada zinazohusiana