Uturuki yataka raia wake kuhama mji wa Karkamis

Moto uliosababishwa na wanamgambo wa kundi la IS
Image caption Moto uliosababishwa na wanamgambo wa kundi la IS

Mamlaka nchini Uturuki zimewataka watu waishio mji wa kusini mwa Karkamis kuondoka baada ya taifa jirani la Syria kukumbwa na moto uliosababishwa na wanamgambo wa kundi la Islamic State.

Mji wa Karkamis upo jirani na mpaka kutokea mji wa Jarablus, ambapo wanamgambo wa IS wapo mji ambao waasi wa wanaoungwa mkono na Uturuki wanajaribu kuuchukua kwa kipindi kifupi.Kundi la waasi lipo kwa wingi katika maeneo hayo.

Image caption Raia wa Uturuki wakionyesha hasira zao kutokana na moto huo

Uturuki imelilaumu kundi la IS kwa shambulizi la kujitoa mhanga na kuuwa watu wengi kusini mwa nchi hiyo mwishoni mwa juma , na kusema kuwa kundi hilo lazima liondoshwe katika maeneo ya mipakani.