Venezuela:Wafanyakazi wanaompinga Rais Maduro kutimuliwa

Rais Nicolas Maduro
Image caption Rais Nicolas Maduro

Mawaziri katika serikali ya Venezuela wamepewa saa 48 kuwatimua kazi wafanyakazi waandamizi wa sekta ya umma ambao walitia saini waraka wa kura ya maoni dhidi ya Rais Nicolas Maduro mapema mwaka huu.

Wito huo wa kura ya maoni ulikuwa na lengo la kumtimua Rais.

Image caption Viongozi wa upinzani wamewataka wananchi kuandamana Septemba 1 kumpinga Maduro

Afisa mwandamizi katika serikali ya Venezuela, Jorge Rodriguez, amesema kwamba serikali yake haiwezi kuwa na watu walio kinyume dhidi ya mapinduzi ya kioshalisti katika nafasi za uongozi.

Nchi Venezuela inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, na uhaba wa bidhaa za muhimu,hali ambayo upande wa upinzani umeelekeza lawama zake kwa serikali ya Rais Maduro.