Biden:Ushahidi unahitajika, Fethullah Gulen kuhukumiwa

Joe Biden (kulia) na waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim mjini Ankara
Image caption Joe Biden (kulia) na waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim mjini Ankara

Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amesema serikali ya Uturuki inahitaji kutoa ushahidi zaidi ili kuhakikisha mhubiri wa kiislam anayeishi Nchini Marekani, anarejeshwa ili ahukumiwe Uturuki baada ya kushitumiwa kuhusika kwenye mapinduzi yaliyoshindwa mwezi uliopita.

Katika kikao chake na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kilichofanyika Ankra, Bwana Biden amesema Marekani haina nia ya kumlinda Fethullah Gulen.

Kwa upande wake bwana Erdogan amesema kuwa mhubiri huyo anapaswa kurudishwa Uturuki haraka iwezekazavyo.

Image caption Biden amesema Marekani haina nia ya kumlinda Fethullah Gulen

Bwana Gulen amekanusha kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi.