Makubaliano yafikiwa kuwaruhusu raia Syria kuondoka Daraya

Hii inatokea baada ya miaka mingi ya kuzingirwa na vikosi vinavyounga mkono serikali.
Image caption Hii inatokea baada ya miaka mingi ya kuzingirwa na vikosi vinavyounga mkono serikali.

Makubaliano yamefikiwa kuwataka raia na waasi waliopo katika eneo la mapigano katika mji wa Daraya baada ya kuzingirwa kwa muda mrefu na vikosi vya serikali ya Syria .

Serikali na mmoja wa makamanda wa makundi ya wapiganaji wamekubaliana kuwa raia na askari wa majeshi ya makundi hayo wanapaswa kuondoka leo eneo hilo .

Vyombo vya habari nchini Syria vimearifu kuwa raia elfu nne na wapiganaji mia saba wataruhisiwa kuondoka eneo hilo.

Image caption Waasi amesema wataanza kuondoka siku ya ijumaa

Vyanzo vya habari vya magharibi vimeiambia BBC kuwa bado hakuna maandalizi ya njia ya salama kwa wapiganaji kutoka katika eneo hilo.

Mji wa Daraya ulio karibu na Damascus tangu mwaka 2012 umezingirwa na vikosi vya serikali na kushuhudia mfululizo wa mashambulizi.

Wakati huo huo mapigano makali yameendelea katika mji wa Aleppo nchini humo pamoja na kuwepo mkazo wa umoja wa mataifa kusitisha mapigano hayo kwa saa 48

Vikosi vya serikali vinadaiwa kuwaua raia 15 kati yao 11 wakiwa ni watoto kufuatia shambulizi dhidi ya waasi karibu na eneo hilo.

Mkuu wa kikosi cha umoja wa mataifa nchini Syria Staffan de Mistura amesema Urusi imekubali kusitisha mapigano ili kutoa nafasi ya kutolewa kwa misaada ya kibidamu,japo makundi makuu ya wapiganaji hayajatoa msimamo wao

Mji wa Daraya umezingirwa na vikosi vya serikali kuanzia mwaka 2012 kufuatia mashumbulizi ya mara kwa mara.