Riek Machar atibiwa Sudan baada ya kutoroka Sudan Kusini

Aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar

Wasaidizi wa kiongozi wa upinzani nchini sudan Kusini , Riek Machar, wanasema kwamba ameruhusiwa kuondoka hospitalini nchini Sudan japo ataendelea kuishi nchini humo.

Bwana Machar alikuwa akitibiwa mguu wake uliokuwa umevimba,kutokana na majeraha iliyopata wakati akitoroka kutoka Sudan Kusini.

Machar anatarajiwa kukutana na rais Omar al-Bashir hivi karibuni.

Machar alifutwa kazi kama makamu wa rais baada ya vita kuzuka upya Sudan Kusini.

Wanajeshi watiifu kwake walianza kupigana na wanajeshi watiifu kwa hasimu wake wa kisiasa rais Salva Kiir.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vikosi vittifu kwa rais Salva Kiir vilikabiliana na vikosi vya aliyekuwa makamu wake Riek Machar

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini vilizuka tena Desemba 2013 kufuatia jaribio la kupindua serikali.

Mapigano yaliendelea hadi kutiwa saini kwa mkataba wa Amani Agosti mwaka jana.

Lakini katika miezi ya hivi karibuni, vita vimezuka upya na aliyekuwa makamu wa rais kuambatana na mkataba huo wa amani, Dkt Riek Machar, akaondoka mji mkuu Juba.