Wahamiaji 300,000 kuwasili nchini Ujerumani

wahamiaji
Image caption Wahamiaji

Mkuu wa idara inayoshughulikia uhamiaji na wakimbizi nchini Ujerumani anasema kuwa anatarajia hadi wahamiaji 300,000 kuwasili nchini humo mwaka huu.

Wakati wa mahojiano na gazeti moja nchini humo, Frank Juergen Weise alisema kuwa ofisi yake itakumbwa na changamoto ikiwa watu zaidi watawasili.

Zaidi ya wahamiaji milioni moja kutoka mashariki ya kati , Afghanistan na Afrika waliwasili nchini Ujerumani mwaka uliopita.

Naye waziri wa mambo ya ndanianchini Ujerumani anasema kuwa zaidi ya watu 390,000 waliomba kupewa hifadhi nchini humo miezi sita ya kwanza ya mwaka huu.

Mada zinazohusiana