Wanamgambo wawatoa jela wenzao Ufilipino

Wanamgambo nchini Ufilipino wanaolitii kundi la Islamic State
Image caption Wanamgambo nchini Ufilipino wanaolitii kundi la Islamic State

Wanamgambo nchini Ufilipino waliotangaza kulitii kundi la Islamic State wamewafungulia kutoka jela wapiganaji wenzao wanane wakati wa uvamizi uliofanywa kwenye gereza moja katika mji ulio kusini mwa Marawi.

Polisi wanasema kuwa takriban wapiganaji 20 kutoka kundi la Maute walivamia gereza la Lanao del Sur Jumamosi usiku na kuwapokonya silaha walinzi.

Wanamgambo hao walikamatwa wiki iliyopita baada ya utawala kuwapata wakisafirisha vilipuzi vya kutengenezewa nyumbani wakitumia gari lao.

Takriban wafungwa wengine15 walitumia fursa hiyo kutoroka jela.

Mada zinazohusiana