Kundi la waasi la FARC kusitisha mapigano Colombia

Image caption Kundi la waasi la FARC limekuwa likipigana tangu mwaka 1964 na kusababisha mamilioni kuwa wakimbizi

Miaka minne baada ya kuanza kwa mazungumzo ya amani, kundi kubwa la waasi nchini Colombia -the FARC- limetangaza kusitisha mapambano na serikali. Kiongozi wa kundi hilo la FARC, ajulikane kama Timochenko, amewaamuru wapiganaji wake wote kusitisha mapigano kuanzia usiku wa kuamkia leo.

Amesema, vita hivyo vya muda mrefu dhidi ya dola vimeisha. Mwandishi wa BBC nchini Cuba amesema tangazo hilo ni la kihistoria kwa kuwa umemaliza mgogoro uliodumu kwa takribani zaidi ya miaka hamsini na kusababisha vifo vya watu laki mbili na elfu sitini na mamilioni kuwa wakimbizi.

Timochenko pia ataitisha mkutano wa mwisho na Kundi lake la FARC ambapo wakala anaewakilisha wapiganaji wa kundi la FARC atadhibitisha mkataba wa amani waliokubaliana na serikali.