Nadal , Keber waanza kwa ushindi michuano ya wazi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rafael Nadal

Nyota wa mchezo wa tenesi Rafael Nadal na Angelique Kerber wameanza vizuri michuano ya wazi ya Marekani iliyoanza jana.

Muhispania Rafael Nadal amemshinda Denis Istomin kwa 6-1 6-4 6-2.Nae Angelique Kerber aliibuka na ushindi wa seti mbili kwa 6-0 1-0 dhidi ya Polona Hercog

Garbine Muguruza nae akamshinda Elise Mertensi kwa 6-0 6-3. Mshindi wa Olympic Monica Puig akachapwa na Zheng Saisai 6-4 6-2

Michuno hii itaendelea tena leo kwa Nyota Serena Williams akichuana na Ekaterina Makarova.huku Mwingereza Andy Murray akicheza na Lukas Rosol.