Serena, Venus washinda katika michuano ya wazi

Serena Williams Haki miliki ya picha Google
Image caption Serena Williams

Ndugu wawili nyota wa mchezo wa tenesi Serena Williams na Venus William wameanza vyema michuano ya wazi ya Marekani.

Serena William anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora kwa upande wa wanawake alipata ushindi wa 6-3 6-3 dhidi ya Ekaterina Makarova.

Nae Venus William alimshinda Kateryna Kozlova kwa seti mbili seti ya kwanza akishinda 6-2,akapoteza seti ya pili kwa 5-7,kisha akamaliza kwa ushindi wa 6-4.