UN: Walinda amani watalindwa dhidi ya Kipindupindu na homa ya manjano

Atul Khare, Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mapema mwezi huu Umaoja wa Matifa hatimae ulikubali kwamba ulichangia katika mlipuko wa Kipindupindu nchini Haiti uliowauwa watu elfu kumi

Umoja wa Mataifa unasema kuwa hatua zinachukuliwa kuchunguza afya ya walinda amani kabla ya kutumwa kufanya kazi katika ujumbe wake, na kuhakikisha wamepatiwa chanjo dhidi ya magonjwa ya kipindu pindu na homa ya manjano.

Atul Khare, ambaye ni naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyasema hayo wakati wa ziara yake nchini Nepal akisisitiza kuwa hatua hizo zitachukuliwa vilevile kwa raia wote.

Mapema mwezi huu Umaoja wa Matifa hatimae ulikubali kwamba ulichangia katika mlipuko wa Kipindupindu nchini Haiti uliowauwa watu elfu kumi kwa kipindi cha miaka sita.

Uchunguzi wa kusayansi umeonyesha kuwa vikosi vya Nepal vilikua chanzo cha ugonjwa uliosambaa kutoka kituo cha Umoja wa Mataifa kupitia mabomba ya uchafu yaliyovuja.