Makao ya Jean Ping yavamiwa nchini Gabon

Kiongozi wa upinzani nchini Gabon Jean Ping aliyeshindwa na Ali Bongo
Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Gabon Jean Ping aliyeshindwa na Ali Bongo

Vikosi vya usalama vimevamia makao makuu ya chama cha mgombea urais aliyeshindwa Jean Ping.

Bwana Ping amekiambia kituo kimoja cha redio kutoka Ufaransa RMC kwamba amekimbia mafichoni kufuatia uvamizi wa makao makuu ya chama chake usiku kucha

Msemaji wa serikali alisema kuwa oparesheni hiyo kwenye mji mkuu Libreville ililenga kuwafurusha wahalifu.

Image caption Wafuasi wa upinzani wakiandamana nchini Gabon baada ya rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais

Alisema wao ndio walihusika katika kuchomwa kwa majengo ya bunge siku ya Jumatano.

Bwana Ping alisema kuwa watu 2 waliuawa wakati wa uvamizi katika makao makuu ya chama.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Ali Bongo wa Gabon

Mapema wafuasi wake waliinga barabarani kupinga tangazo kuwa rais Ali Bongo alishinda uchaguzi kwa chini ya kura 6000.

Kwa sasa kiongozi huyo wa upinzani amedai kuwa anahofia usalama wake na kwamba huenda akakamatwa muda wowote.