Marcel Lazar, mdukuzi wa watu maarufu adakwa Marekani

Marcel Lazar Haki miliki ya picha Reuters
Image caption mdukuzi wa mambo binafsi ya watu maarufu adakwa Marekani

Mahakama moja nchini Marekani imemfunga jela raia moja mwenye asili ya nchini Romania kwa kosa la udukuzi mtandaoni kwa watu wenye hadhi za juu nchini humo ikiwemo familia ya Bush.

Marcel Lazar, alikuwa akitumia mfumo wa "Guccifer", kutekeleza udukuzi huo, amefungwa jela kwa muda wa miezi hamsini na mbili. Mwendesha mashtaka alisema Marcel aliidukua akaunti ya barua pepe ya Familia ya Bush naku baini picha binafsi zenye kushikamana na marais wa zamani, George H.W.Bush na George W. Bush.

Wakati wa mahojiano na mtuhumiwa huyo, alisema alivunja mfumo wa komputa binafsi uliokuwa ukitumiwa na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic Hillary Clinton, wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, hata hivyo kitengo cha usalama wa kimtandao nchini humo umepinga madai hayo.

Marcel alifikishwa nchini Marekani mwezi Aprili na kukutwa na hatia ya kuingilia mifumo binafsi ya watu ya komputa zilizokuwa na ulinzi binafsi .