Utafiti umebaini kuwa huenda watu bilioni 2 wakaambukia virusi vya Zika

Mbu aina ya Aedes aegypti Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Mbu aina ya Aedes aegypti anafahamika kueneza virusi vya Zika

Zaidi ya watu bilioni mbili wanaweza kuwa katika hatari ya mlipuko wa virusi vya Zika katika baadhi ya maeneo ya Afrika na Asia, kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye jarida la masuala ya kitabibu la Lancet.

Wakazi wa nchi za India, Indonesia na Nigeria ni baadhi ya wale walio katika hatari ya kupata maambukizi zaidi ya virusi vya Zika, utafiti umesema.

Walitumia taarifa kutoka kwa watu wanaotumia usafiri wa ndege kusaidia katka makadirio yao.

Hata hivyo wamebainisha kwamba, kinga kwa virusi hivyo inaweza kuwepo katika baadhi ya maeneo na hivyo kuweza kupunguza hatari.

Jopo la watafiti kutoka chuo cha masuala ya usafi na tiba ya magonjwa ya maeneo yenye joto cha London, Chuo Kikuu cha Oxfordna kile cha Toronto, nchini Canada, wanasema " Watu wa wengi " miongoni mwa watu wanaishi katika mazingira ambako itakuwa vigumu kuzuia, kubaini na kushughulikia virusi vya Zika.

Waliangalia masuala kama vile idadi ya watu wanaosafiri kutoka maeneo yaliyoathiriwa na Zika ya Amekika Kusini kuelekea Afrika na Asia, uwezo wa mbu ambao wanaweza kusafirisha virusi na hali ya hewa katika kanda hizo katika kutathmini ni nchi gani inayoweza kuwa na hatari ya mlipuko wa huo.