UN yataka vyombo vya habari kulindwa Somalia

Waandishi wa Somalia wakiandamana kufungwa kwa mwenzao
Image caption Waandishi wa Somalia wakiandamana kufungwa kwa mwenzao

Umoja wa Mataifa unasema lazima zifanywe juhudi zaidi za kulinda uhuru wa vyombo vya habari nchini Somalia, ambako waandishi wa habari 30 wameuwawa katika miaka mine iliyopita.

Shirika la kutetea haki za kibinaadamu la Umoja wa Mataifa, linasema katika ripoti yake, kwamba tangu mwaka wa 2014, waandishi wa habari mia 120 wengine wamekamatwa kiholela.

Vyombo vya habari kadhaa vimefungwa.

Ripoti hiyo imetaka haki ya kujieleza iheshimiwe, kabla ya uteuzi wa bunge jipya baadae mwezi huu.

Inasema wabunge 18 wameuawa tangu 2012, na wanaharakati kadha wa kisiasa wamefungwa.

Waandishi wa wanasiasa wamekuwa wakiuawa na wapiganaji wa kundi la al Shabab pamoja na wapinzani ambao wanapinga kazi yao.