Mkutano wa G20 waendelea nchini China

Idadi ya mikutano baina ya nchi tayari imeshafanyika na masuala mbalimbali ya siasa yamejadiliwa
Image caption Idadi ya mikutano baina ya nchi tayari imeshafanyika na masuala mbalimbali ya siasa yamejadiliwa

Viongozi wa nchi 20 zenye uchumi mkubwa duniani wameingia siku ya pili ya mazungumzo huko China.

Rais wa China Xi Jinping amewataka viongozi kufanyia kazi malengo ya muda mrefu ya kukuza maendeleo ya uchumi.

Amesema pia jitihada zaidi zinahitajika kuhakikisha kuwa manufaa ya utandawazi yanafaidisha wote pamoja na uchumi, usalama, na vita dhidi ya ugaidi vinajadiliwa.

Idadi ya mikutano baina ya nchi tayari imeshafanyika na masuala mbalimbali ya siasa yamejadiliwa.

Vyombo vya habari vya China vinasema kuwa katika mkutano na Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye, Rais Xi amesema China kuipinga marekani juu ya nia yake ya kupeleka mfumo wa kupambana na makombora huko Korea ya kusini, inaweza kusababisha mgogoro.