Biashara na uwekezaji wasisitizwa katika mkutano wa G20

G20,China Haki miliki ya picha BBC chinese
Image caption mkutano wa G20, China

Mkutano wa mwaka wa G20 unaojumuisha mataifa yenye uchumi mkubwa duniani umemalizika nchini China, ukiongozwa na Rais Xi Jinping, amesema wajumbe wa nchi wanatakiwa kuimarisha nguvu mbili za kibiashara na uwekezaji.

Akiongea huko Hangzhou, Rais Xi amesema kutakuwa na makubaliano kupinga ulinzi wa soko. Amesema kuwa kwa mara ya kwanza mkutano huo umeweka masuala ya maendeleo mbele na kati.

Mkuu wa IMF, Christine Lagarde, amesema viwango vya ukuaji uchumi duniani umekuwa ukishuka kwa muda mrefu na wajumbe wa G-20 watatumia kila njia kuukuza.

Na tamko la mwisho limekubaliana na mataifa kuongeza usaidizi wa ubinadamu na na misaada kwa wakimbizi.