Wayne Rooney akerwa na mjadala juu yake

kaptein
Image caption Wayne Rooney

Kapteni wa timu ya Uingereza Wayne Rooney amesema kuwa majadiliano yanayoendelea kuhusu shughuli zake ndani ya timu hayana maana.

Rooney ambaye amecheza mechi yake ya 116, akicheza kama kiungo siku ya jumapili walishinda 1-0 dhidi ya slovakia, ambayo ilikuwa ni mechi ya kwanza chini ya meneja mpya Sam Allardyce's.Allardyce amesema kuwa mechi iliyopita hakuwa na la kusema kuhusu nafasi ya Rooney ilikuwa ipi na kucheza alivyotaka.

Rooney mwenye miaka 30 alisema " Nilicheza kwa nafasi yangu ili kusaidia timu yangu kushinda mchezo, japo mengi yalifanyika juu yake"

Akiongea na Sky Sport, kapteni wa timu ya Manchester United aliongeza kuwa" Nimekuwa nikifanya kazi yangu yote na ghafla ikawa habari kubwa, si jambo kubwa na nadhani kuna kutoeleweka kwa kiasi kikubwa juu ya hilo"

Nafasi ya Rooney kwenye Klabu yake na nchi imekuwa ikijadiliwa kwa kiasi kikubwa msimu huu na kwa rekodi ya wafungaji nchini Uingereza.