WHO yatoa mwongozo wa ugonjwa wa Zika

zika
Image caption wafanyakazi wa kudhibiti ugonjwa wa Zika

Shirika la Afya la Duniani WHO, limetoa mwongozo mpya kwa watu ambao walizuru maeneo yalioathirika na Virusi vya ugonjwa wa Zika.

Ushauri mpya ni kuwa wanaume na wanawake wanaorudi kutoka kwenye maeneo hayo, wanatakiwa wafanye ngono salama au kutofanya kabisa kwa muda wa miezi sita bila kujali kama kuna dalili za virusi au kujaribu kubeba mimba.

Virusi hawa wa zika wanaweza kusababisha watoto kuzaliwa na wakiwa na maendeleo duni ya ubongo, ambapo wanaenezwa na mbu, lakini unaenezwa kwa uharaka na kwa njia ya ngono kuliko njia iliyodhaniwa hapo awali.

Mwezi Juni shirika la Afya Duniani WHO, lilitoa mwongozo sawia, lakini ilikuwa kwa wanaume tu, na kupendekeza muda wa wiki nane.