Australia bingwa wa mpira wa magongo kimataifa

akifurahia ushindi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Glenn Maxwell

Australia imeweka rekodi mpya ya ushindi kwenye mashindano ya kimataifa ya mpira wa magongo maarufu kama Twenty20 baada ya kuishinda Sri Lanka kwa 263-3 huko Pallekele. Jumla ya mipigo 260 iliwekwa na Sri Lanka dhidi ya Kenya mwaka 2007 Glenn Maxwell nae alipiga mipigo 145 na kutoa nje mipira 65.

Sri Lanka ilishinda kete na kuchaguliwa kuwa ya kwanza ambapo iliweza kuhimili seti 178-9 kwa kuwajibu Austraria walioshinda mchezo wa kwanza kati ya miwili iliyofuatana kwa mizunguko 85. Maxwell, ambaye alifungua mapambano, na kushinda kwa seti 9- 6 na 14-4 ambayo ni ya pili kwa ukubwa kwenye mashindano ya cricket ya kimataifa maarufu kama T20.

"kwa utaratibu ukiwa juu unapata uhuru mwingi zaidi kwenye mchezo na kucheza kwa tahadhari."Maxwell alisema. Maxwell.Mchezaji mwingine Aaron Finch anashikilia rekodi yake ya kushinda 156, ambayo alishinda dhidi ya England mwaka 2013.

Japo kuwa Maxwell mwenye umri wa miaka 27 anacheza michuano ya wazi baada ya Finch kuvunjika kidole kwenye mchezo dhidi ya Sri Lanka uliofanyika hivi karibuni dhidi ya Ufaransa."kusalia juu ni mahali fulani ningependa kubaki, lakini kwenye timu nyingi nilizozichezea sikupata fursa", alisema Maxwell.

Rekodi ya Australia kwenye michuano ya T20 imekuja siku nane tu baada ya England kuweka rekodi mpya siku moja kwenye michuano ya kimataifa ya Cricket, 444 dhidi ya pakistan ambayo iliweka rekodi katika michuano iliyopita dhidi ya Sri Lanka.