Michuano ya Olimpiki kwa walemavu ni leo Rio de Janeiro

paralimpics olimpic
Image caption Moja ya burudani mjini Rio de Jeneiro

Michuano ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu inatarajiwa kuanza hivi leo mjini Rio de Janeiro nchini Brazil. wataandaaji wa michuano hiyo wameahidi kuwepo kwa shamra shamra za kila namna katika sherehe za ufunguzi za michuano hiyo, ambayo lengo lake ni kuleta changamoto kwa watu wenye mitizamo tofauti kwa walemavu na hivyo kupitia michuano hiyo, dhana hiyo itatupiliwa mbali kutokana na uwezo utakaaoneshwa na wachezji wa jamii ya walemavu.

Moja ya changamoto kubwa katika michuano hiyo ya Olimpiki ni kugubikwa na mgogoro wa kifedha pamoja na mauzo ya tiketi za ufunguzi wa michuano hiyo kwenda mwendo wa kobe.

Michuano hiyo inatarajiwa kushirikisha wanariadha zaidi ya elfu nne kutoka mataifa mia moja na sitini ulimwenguni watakao kuwa katika gwaride la ufunguzi,ingawa miongoni mwa hao wanariadha wa kutoka nchini Urusi hawamo.

Wanamichezo wa Urusi wamepigwa marufuku kushiriki katika michuano hiyo kutokana na wasiwasi wa utumizi wa dawa za kusisimua misuli ambazo zilipigwa marufuku michezoni, inaelezwa kuwa sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo zitashuhudiwa na mamilioni ya watu ulimwenguni kote.