Fifa yazuia usajili Real Madrid na Atletico Madrid

Hispania
Image caption Atletico Madrid wakipokea maelezo, mazoezini

Shirikisho la soka duniani , FIFA limezipiga marufuku timu za Real Madrid na Atletico Madrid kusajili wachezaji wapya.Zuio hilo linadaiwa kudumu mpaka mapema mwaka 2018.

Klabu hizo za nchini Hispania zimekata rufaa kufuatia amri hiyo ya FIFA iliyotolewa mwezi January mwaka huu ya kwamba wamevunja taratibu na sheria wakati wa usajili wa chipkizi kutoka nje.

Timu ya Real Madrid imeielezea hatua hiyo kama ukiukwaji wa haki na imeeleza dhamira yake ya kukata rufaa zaidi, katika mahakama ya Usuluhishi ya Michezo.