Roboti yafanya upasuaji wa macho mara ya kwanza duniani

Image caption Roboti hiyo ilitumia sindano nyembaba kuondoa ngozi kutoka jicho la mgonjwa

Madaktari wametumia roboti ya kwanza kufanya upasuaji wa macho na kurejesha uwezo wa kuona kwa mgonjwa kwa mara ya kwanza duniani.

Kundi la madaktari kutoka hospitalia ya John Radclife nchini Uingereza, walitumia roboti hiyo kutoa ngozi nyembamba zaidia kutoka jicho la mgonjwa.

Mgonjwa kwa jina Bill Beaver mwenye umri wa miaka 70 aliyefanyiwa upasuaji huo sasa anasema anahisi vyema.

Madaktari wana matumaini kuwa mfumo huo utasaidia katika upasuaji unaohitaji umakini zaidi.

Image caption Roboti hiyo ilitumia sindano nyembaba kuondoa ngozi kutoka jicho la mgonjwa