Marekani yaadhimisha shambulio la Septemba 11

Shambulio la Septemba 11 2001 nchini Marekani
Image caption Shambulio la Septemba 11 2001 nchini Marekani

Marekani inaadhimisha mwaka wa kumi na tano tangu shambulio la wapiganaji wa jihad la Septemba 11 ambalo liliwaua watu 3000 na kusababisha vita dhidi ya wapiganaji wa kigaidi duniani.

Katika ikulu ya rais ,rais Obama ataadhimisha shambulio hilo mida ya saa 2 na dakika 46 alfajiri wakati ambapo ndege iliotekwa nyara iligonga jumba refu la World Trade Center mjini New York,na kuanzisha vita vikali dhidi ya magaidi nchini Marekani.

Baadaye majina ya waathiriwa wote yatasomwa katika ibada ya kumbukumbu katika eneo la Ground Zero ambapo jengo la WTC lilianguka.

Shambulio hilo la Septemba 11 lilisababisha uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq,na lilisababisha mashambulio zaidi ya kigaidi kutoka Bali hadi Brussels.