Aliyewaita watu weusi nyani apigwa faini Afrika Kusini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Alisema aliwaita hivyo kutokana na fujo walizokuwa wamezua katika fuo za Durban

Mahakama nchini Afrika Kusini imempiga faini mwanamke mmoja mzungu ambaye aliwaita watu weusi nyani na kuzua ghadhabu nchini humo, jumla ya dola 344 au atumikie kifungo cha mwaka mmoja jela. Pia ametakiwa aombe msamaha.

Penny Sparrow alitumia jina hilo kuwaelezea watu waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya katika fuo za mji wa Durban kutokana na fujo walikuwa wamesababisha.

Alikosolewa na wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Alijaribu kujielezea kwenye mahojiano ya runinga akisema kuwa alifanya makosa kuwafananisha watu weusi na nyani, akisema kuwa alifanya hivyo kwa sababu anapenda wanyama.