Wanaopinga kuondolewa umri wa kustaafu majaji wakamatwa Uganda

Image caption Polisi wenye silaha walitumwa eneo la ukumbi wa kitaifa wa sanaa

Polisi wa kupambana na ghasia nchini Uganda wametumwa kwenda kwa ukumbi wa kitaifa sanaa mjini Kampala ambapo kundi la waanawake 30 walikusanyika kufanya maandamano.

Wanawake hao walikuwa na nia ya kutembea hadi majengo ya bunge, kupinga mswada ambao una lengo la kufanyia katiba mabadiliko, kuondoa miaka ya majaji kustaafu ambayo kwa sasa ni miaka 75.

Waandamanaji wana hofu kuwa ikiwa miaka ya majaji kustaafu itaondolewa utakuwa pia ndio mwanzo wa kundoa miaka ya kustaafu kwa rais.

Image caption Wanapinga kuondolewa umri wa kustaafu kwa majaji ambayo ni miaka 75

Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliye na umri wa miaka 72, na ambaye ameongzoa nchi tangu mwaka 1986 hawezi kuruhusiwa kuwania urais kwa muhula wa sita mwaka 2021 chini ya sheria za sasa.

Malori yaliyowabeba polisi waliojihami vikali yalizingira majengo hayo ya ukumbi ya sanaa

Wanawake hao waliokuwa wamevalia nguo nyeupe ishara ambayo ni amani, kisha walijazwa ndani ya malori ya polisi na kuchukuliwa.