Ajali yaikumba meli kubwa zaidi duniani

Haki miliki ya picha PA
Image caption Meli ya Harmony ndiyo kubwa zaidi duniani na inaweza kuwabeba zaidi ya abiria 8000

Mhudumu mmoja ameuawa na wengine wanne kujeruhiwa, wawili vibaya, baada ya ajali iliyohusisha mashuo ya kukoa maisha kwenye meli ya Harmony ambayo ndiyo kubwa zaidi duniani.

Wakati meli hiyo ilisimama kati mji wa Marseille, wahudumu wake wanaripotiwa kushiriki katika mazoezi ya kiusalama wakatimashua hiyo ilichomoka kutoka kwa ghrofa ya tano

Meli ya Harmony inaweza kubeba zaidi ya abiria 8000 pomoja na wahudumu.

Meli hiyo yenye urefu wa zaidi ya nyumba ya ghorofa tano, ilianza kuhudumu mwezi Mei mwaka huu.