Mapigano yaanza upya Syria, baada ya mkataba kumalizika

Magari ya misaada nchini Syria Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Magari ya misaada nchini Syria

Ndege za kivita nchini Syria zimeanza kushambulia mji wa Aleppo muda mfupi tu, baada ya jeshi kutangaza kumalizika kwa wiki ya kusimamisha mapigano.

Wanaharakati wanasema kuna watu waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulio hayo ya anga katika eneo linaloshikiliwa na waasi, la Aleppo na vijiji vya jirani.

Aidha wamesema kuwa malori ya misaada yaliyokuwa karibu na mji huo pia yameshambuliwa.

Majeshi ya Syria na yale ya waasi yamekuwa yakilaumiana kukiuka hatua hiyo ya kusimamisha mapigano.

Marekani imesema inafanyia kazi suala la kuongeza muda wa kusimamisha mapigano.