Upinzani walalamikia Upungufu wa chakula Venezuela

Wapinzani nchini Venezuela Haki miliki ya picha Wales News Service
Image caption Wapinzani nchini Venezuela

Gavana wa jimbo la Miranda nchini Venezuela, Henrique Capriles, ametangaza kuwepo kwa upungufu wa chakula katika eneo lake.

Amesema hali hiyo inasababishwa sera ya serikali.

Capriles ambaye ni kiongozi maarufu wa upinzani nchini humo, amesema, sera za uchumi za Rais Nicholas Maduro zimewaacha na njaa watoto na wazee.

Alikuwa akiisisitizia serikali kurejesha mfuko wa malipo kwa wanafunzi kwa ajili ya chakula, lakini hata hivyo bado hajapokea majibu.

Rais Maduro amewarushia lawama wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda binafsi kwa kusababisha upungufu wa Chakula nchini Venezuela.