Kiwango cha riba katika mikopo kimepunguzwa Kenya

Gavana wa benki kuu Kenya Patrick Njoroge Haki miliki ya picha CENTRAL BANK OF KENYA
Image caption Gavana wa benki kuu Kenya Patrick Njoroge

Katika hata ambayo haikutarajiwa, Benki kuu nchini Kenya imekata kiwango chake cha riba kwa mikopo kutoka asilimia 10.5 hadi asilimia 10.

Ni kiwango cha chini kushuhudiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kutokana na wasiwasi kuhusu kupungua kwa ukuwaji wa mikopo katika sekta binafsi, uamuzi huo unajiri wiki moja baada ya sheria mpya ilioidhinisha viwango vipya vya riba kwa mikopo katika taifa hilo tajiri Afrika mashariki.

Wanauchumi hawakulitarajia hilo. Walitabiri kwamba hakutokuwana na tofauti hadi mwezi Novemba, kwasababu hapakuwa na mabadiliko mazito katika uchumi wa taifa.

Kamati inayohusikana sera kuhusu masuala ya fulusi inasema ni sawa kupunguzwa kwa kiwango hicho cha riba kutokana na kupungua kwa bei za bidhaa, sarafu kuimarika na kushuka kwa bei za mafuta.

Hatua hii imenuiwa kukuza uwekezaji katika sekta binafsi, lakini mabenki yanasema yanahitaji kiwango cha juu cha riba kutokana na hatari ya kukopesha katika masoko yanayoinukia Afrika.

Wakati hatua hii huenda ni ushindi kwa wanliochukua mikopo, kuna wasiwasi kwamba itawasukuma watoaji mikopo kusitisha mikopo kwa watu wanao waona kuwa katika hatari ya kutolipa.