Afisa wa polisi ashtakiwa Tulsa kwa mauaji.

Afisa Betty Shelby (kushoto) alimuua Terence Crutcher, kwenye picha na pacha wake

Chanzo cha picha, POLICE HANDOUT, CRUTCHER FAMILY

Maelezo ya picha,

Afisa Betty Shelby (kushoto) alimuua Terence Crutcher, kwenye picha na pacha wake

Afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua mwendesha gari mweusi Tulsa, Oklahoma, ameshtakiwa kwa mauaji, mwendesha mashtaka mmoja amesema.

Afisa Betty Shelby amempiga risasi na kumuua Terence Crutcher wiki iliopita alipkuwa amesimama karibu na gari lake lililoharibika.

Huko Charlotte, North Carolina, marufuku ya kutotoka nje imeanza kufanya kazi kuzuia ghasia kwa usiku wa tatu baada ya kuuawa kwa mwanamume mwingine mweusi na afisa wa polisi mweusi.

Familai ya Keith Lamont Scott inakana tuhuma za polisi kuwa alikuwa amejihami.

Waandamanji waliokusanyika kupinga mauaji ya Bwana Scott huko Charlotte wamekaidi amri hiyo ya kutotoka nje - inayoanza saa sita usiku hadi kumi na mbili alfajiri, baadi wakisalia barabarani wakiimba nyimbo za injili .

Kwa mujibu wa Cpt Mike Campagna, maafisa hawakutumia nguvu kuidhinisha marufuku hiyo ya kutotoka nje kwa sababu maandamano hayo kwa ukubwa yalikuwa yamani.

Chanzo cha picha, @CMPD

Maelezo ya picha,

Ujumbe wa polisi katika mtandao wa Twitter

Hatahivyo polisi Charlotte wameripoti kuwa maafisa wawili wamejeruhwa Alhamisi usiku.

Mamia ya maafisa wa jeshi wametawanywa barabarani.

Baadi ya waandamanaji wanataka kuona kanda ya video ya mauaji hayo iliotolewa kwa familia ya bwana Scott pekee.

Polisi mpaka sasa wamekataa kuitoa kanda hiyo ya video kwa umma.

Wanasema Keith Lamont Scott alikataa kuiangusha bunduki yake lakini familia yake inasema hakujihami na badala yake alikuwa amebeba kitabu.