Bei za Taxi zaangushwa tena na washindani wapya!

Taxi Mtandaoni Haki miliki ya picha PA
Image caption Uber ndio waliochochea ujio huo wa Taxi za bei nafuu.

Kampuni nyengine ya kutoa huduma za bei nafuu za taxi kupitia mtandao wake Mondo Ride imepunguza bei zake na kuziweka kiwango cha 1/5 ikilinganishwa na zile zilizoko sasa.

Ushindano huo sasa unawapa watoa huduma wengine wa Taxi changamoto kubwa kwani kampuni ya Uber,tayari ilikuwa imepunguza bei kwa theluthi moja tangu mwezi July.

Kwa mujibu wa mpangilio wa bei uliotolewa na kampuni hiyo ya Mondo Ride iliyo na makao yake huko Dubai, wateja watalipa bei ya KSh45 kwa kilomita na kuongezea Ksh 3 kwa kila dakika, kwa bei ya awali ambayo ni Ksh100, na hayo yataanza kutekelezwa hapo usiku wa kuamkia Ijumaa.

Awali Mondo Ride ilikuwa ikitoza hiyo bei ya Sh 100 na kuongezea Sh58 kwa kilomita na Sh4 kwa kila dakika inayoongezeka kwenye safari ya mteja.

Kampuni hiyo inasema ina karibu madereva 1,000 nchini Kenya, na inakuwa ya pili kupunguza bei zaidi, baada ya kampuni ya Taxify kutangulia kufanya hivyo.

Uber ndio waliochochea ujio huo wa Taxi za bei nafuu.

Taxify, kampuni ya huko Estonia hapo mwezi wa 8 waliapunguza bei kwa kiwango cha kutoka Sh50 hadi 40 kwa kilomita, na kutoka Sh 5 hadi 4 kwa dakika ,kando na zile za awali za ada ya Sh100.

"Lazima twende na mtindo wa soko unavyokwenda ," Mkuu wa Mondo Ride Africa Joar Lindh,amenukuliwa kusema.