Mshike mshike wa EPL kuendelea

Rooney Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wayne Rooney wa Man United

Ligi kuu ya England inaendelea Jumamosi kwa nyasi za viwanja vinane kuwaka moto, mchezo wa mapema utawakutanisha Mashetani Wekundu wa Manchester United watakua katika dimba lao la Old Traford kuwaalika mabingwa watetezi wa ligi hiyo Leicester City.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexi Sanchez wa Arsenal

Mchezo mwingine mkubwa kwa siku ya leo ni ule wa Arsenal watakaokua wanakipiga na Chelsea mchezo utakaochezwa katika dimba la Emirates.

Haki miliki ya picha EPA

Majogoo wa Anfield Liverpool watashuka dimbani kuwaalika Hull City.

Vijana wa Aitor Karanka Middlesbrough wao watakua na kibarua pevu cha kuwakabili Tottenham Hotspur waliko chini ya kocha Mauricio Roberto Pochettino.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kevin De Bruyne wa Man City

Swansea City wenye mwendo wa kusua sua watakua nyumbani katika dimba la Liberty kuwakaribisha matajiri wa Manchester City.

Paka weusi wa Sunderland wenye mwanzo mbaya wa ligi watacheza na Crystal Palace, Huku Stoke City wakipepetana na West Bromwich Albion.