Big Sam abwaga manyanga England

England Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa timu ya taifa ya England Sam Allardyce, ama Big Sam, ameachia ngazi

Kocha wa timu ya taifa ya England Sam Allardyce, ama Big Sam, ameachia ngazi kuendelea kuinoa timu hiyo timu ya taifa.

Kung'atuka huku, kumesemwa ni kwa makubaliano ya pande mbili, na kumekuja baada ya Gazeti la Uingereza la The Daily Telegraph,kudai kocha huyo alizungumzia njia zisizo halali za umiliki wa upande wa tatu kwa wachezaji.

Gazeti hilo limechapisha habari kuwa kuna maripota waliojifanya wafanyabiashara walizungumza na Kocha huyo na yeye alikiri inawezekana kuizunguka Sheria ya Chama cha Soka England, ya mwaka 2008 ya kuzuia Mchezaji kuwa na mmiliki mwingine wa Kibiashara mbali ya Klabu yake.

Big Sam amekua kocha wa timu ya taifa kwa siku 67 na kuingoza katika mchezo mmoja tu, chama cha soka cha England FA imetamka Gareth Southgate kuwa kocha wa muda wa kikosi cha nchi hiyo