Urusi yaionya Marekani na kuitaka isiishambulie Syria

Image caption Mji wa Aleppo umekuwa ukishambuliwa mara kadha

Urusi imeionya Marekani isichukue hatua yoyote ya kijeshi, dhidi ya wanajeshi wa serikali ya Syria.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Moscow, alieleza kwamba kuingilia kati kwa namna hiyo, kutasababisha yale aliyoeleza kuwa matokeo yatayotikisa Mashariki ya Kati nzima.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marekani inamtaka Rais Assad aondoke madarakani

Alisema, iwapo mshirika wa Urusi nchini Syria, Rais Bashar al-Assad, atatolewa madarakani, kutafuata pengo, ambalo haraka, litajazwa na magaidi.

Matamshi hayo yametolewa wakati wa mvutano mkubwa baina ya Urusi na Marekani, kuhusu mashambulio ya mabomu yanayoendelea, dhidi ya Aleppo.