Uingereza kuondoka katika EU mwaka ujao

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May
Image caption Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa Uingereza itaanza kujiondoa rasmi katika muungano wa Ulaya mwishoni mwa mwezi Machi mwaka ujao.

Alikuwa akizungumza na BBC kabla ya kufanyika kwa mkutano wake wa kwanza kama kiongozi wa chama cha kihafidhina.

Katika mkutano huoi May amesema atazindua sheria mpya mwaka ujao ili kulifanya taifa la Uingereza kuwa huru tena.

Katika mahojiano na gazeti la Sunday Times, MAY amesema sheria iliyoipeleka Uingereza kwa muungano wa Ulaya, itabadilishwa na kwamba nguvu itarudishwa kwa taasisi zilizochaguliwa nchini humo.

Hata hivyo hilo halitafanyika hadi pale Uingereza itakapo ondoka rasmi kutoka kwa muungano wa ulaya.

Matamshi ya Bi May yanakuja kabla ya kuandaliwa kwa mkutano mkuu wa kila mwaka wa chama cha Conservative.