Wanafunzi warushiwa maguruneti Afrika kusini

Vyuo vikuu vingi vimefungwa Afrika kusini kutokana na maandamano Haki miliki ya picha EPA
Image caption Vyuo vikuu vingi vimefungwa Afrika kusini kutokana na maandamano

Polisi wengi katika chuo kikuu cha Wits huko Johannesburg wametumia maguruneti ya kutawanya waandamanaji kusitisha maandamano dhidi ya wanafunzi na wanaharakati wanaotaka kuwe na elimu ya bure kwa kila mtu.

Vyuo vikuu vingi Afrika kusini vimefungwa katika wiki mbii zilizopita kutokana na ghasia.

Wanafunzi kadhaa wamekamatwa kwa kukiuka agizo la mahakama lililowazuia kukusanyika katika makundi ya watu zaidi ya 15 katika vyuo hivyo.

Kiongozi wa wanafunzi Busisiwe Seabe pia alikamatwa.

''Nimekamatwa kwa kuuliza maswali'' aliwaambia waandishi habari akiwa nyuma ya gari la polisi.

Chuo kikuu cha Wits kimetangaza Jumatatu kuwa mafunzo yataanza upya wiki hii kufuatia matokeo ya kura amapo wanafunzi wengi waliunga mkono kufanya mtihani katika wiki zijazo.

Naibu chancellor Adam Habib amesema huenda mafunzo ya mwaka huu yakasita iwapo wanafunzi hawatorudi darasani Jumanne.

Ameongeza kuwa wanafunzi hawatofuzu na chuo hicho hakitowasajili wanafunzi apya katika mwaka mpya.