Mwizi aonekana katika kamera akiiba fedha za hisani

Mwizi aliyeiba kikapu cha fedha za hisani apatikana katika kamera Edinburgh Haki miliki ya picha TAPA
Image caption Mwizi aliyeiba kikapu cha fedha za hisani apatikana katika kamera Edinburgh

Mwizi mmoja amepatikana katika kamera za CCTV akiiba kikapu cha fedha za hisani katika mkahawa mmoja huko Edinburgh.

Kanda hiyo ya Video inamuonyesha mtu huyo akichukua fedha hizo za hazina ya Daisy Chain kutoka kwa mkahawa huo wa Tapa on Shore place,Leith.

Mara ya kwanza wenye mkahawa huo walidhani kikapu hicho kilikuwa kimewekwa mahali kisipostahili kuwa ,lakini wakaangalia kamera hiyo ya CCTV waliposhindwa kukiona wiki mbili baadaye.

Tayari maafisa wa polisi wanatafuta mashahidi wa wizi huo uliofanyika mnamo tarehe 20 mwezi Septemba.

Kulikuwa na takriban paundi 90 katika kikapu hicho.

Mmiliki wa mkahawa huo wa Tapa ,Daniel Shearon amesema kuwa wafanyikazi waliokuwa kazini walikuwa katika afisi ya nyuma wakati wizi huo ulipotendeka.